Waziri Mkuu wa Libya Abdullah
al-Thinni amesema amenusurika jaribio la kuuwawa na watu wenye silaha
walioshambulia gari lake katika mji wa Tobruk.
Akiongea na televisheni ya habari ya
al-Arabiya al-Thinni amesema anamshukuru Mungu kumuepusha na risasi
zilizolenga gari lake wakati akitoka kwenye kikao cha bunge.
Msemaji wa serikali ya Libya amesema
waziri mkuu hakupata jeraha lolote katika shambulio hilo ila mmoja wa
walinzi wake amejeruhiwa.
Nchi ya Libya imekuwa kwenye
machafuko tangu Muammar Gaddafi ang'olewe madarakani mnamo mwaka
2011.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni