Idadi ya vifo vinavyotokana na joto
kali nchini India vimepita zaidi watu 1,000 huku hali ya joto
ikikaribia nyuzi joto 50 katika baadhi ya maeneo.
Vingi ya vifo vimetokea katika jimbo
la kusini la Telangana pamoja na Andhra Pradesh, ambapo watu 1,118
wamekufa tangu wiki iliyopita.
Ripoti zinaeleza watu wengine 24
wamekufa kutokana na joto kali huko Bengali Magharibi pamoja na
Orissa. Hali ya joto hilo inatarajiwa kupungua katika siku chache
zijazo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni