Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ndugu Isaya M. Mngurumi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo akiwa na Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena wakiwa wanatoa maelezo juu ya uzoaji na usindikaji wa Taka zinazokusanywa katika sehemu mbalimbali za Manispaa ya Ilala na jinsi ya watakavyoyatumia magari hayo yaliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
Akizungumza wakati wakati wa tukio la uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi ya Kampuni iliyopewa zabuni kusafisha manispaa ya Ilala, Green Waste Pro Ltd Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi amesema kushirikiana vyema kwa kampuni Green Waste Pro Ltd ndiko kunako pelekea maendeleo na afya bora katika manispaa ya Ilala hivyo tuwaunge mkono wenzetu kwa kuwapa ushirikiano wa kuto tupa taka hovyo bali maeneo husika yaliyo wekwa kwaajili ya kuhifadhi taka hizo ili waweze kuzipitia kwa urahisi na kuzipeleka mahala panapo husika.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni