.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 2 Mei 2015

NANI KUIBUKA MBABE WA MWENZAKE KESHO ALFAJIRI KATI YA PACMAN AU MAYWEATHER

Mabondia Floyd Mayweather ( kushoto ) na Manny Pacquiao walipokutana wakati wa kupima uzito jana ijumaa kabla ya pambano lao liltakalopigwa kesho alfajiri.
                                                                    Floyd Mayweather akipima uzito
                                                                        Manny Pacquiao akipima uzito. 

Mabondia Manny Pacquiao na mpinzani wake Floyd Mayweather jana wamepima uzito kabla ya pambano lao linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa mchezo huo kote ulimwenguni, pambano ambalo litapigwa kesho alfajiri. 

Pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa MGM Grande Garden Arena mjini Las Vegas nchini Marekani. Mabondia wote kila mmoja ametamba kuibuka na ushindi dhidi ya mwenzake. 

Mayweather raia wa Marekani ana umri wa miaka 38, ana urefu wa futi 5.8 na katika rekodi ya mapambano yake, ameshinda yote 47, hajawahi kupigwa. 

Kwa upande wa Manny Pacquiao maarufu kama Pacman raia wa Ufilipino, ana umri wa miaka 36, ana urefu wa futi 5.6. 

Katika mapambano aliyopigana, ameshinda mara 57, amepigwa mara 5 na sare mara 2.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni