Maafisa wa Mamlaka ya Dawa nchini
Uganda wamepigwa na butwaa baada ya kumkuta muuguzi wa kike akiwa
katika hali ya mahaba na mgonjwa wake kwenye chumba cha matibabu
katika Zahanati moja wakati wakifanya ukaguzi wa kushtukiza.
Muuguzi huyo aliyefahamika kama
Lillian Ntegeka, anayefanyakazi katika Zahanati ya All Saints Clinic
katika mji wa Hoima, alikutwa katika hali hiyo akiwa na mwanaume
aitwae Lee Wandera juu ya kitanda cha matibabu, ambapo baadae alidai
kuwa ni mpenzi wake.
Maafisa wa Mamlaka ya Dawa wa Uganda
walikasirishwa mno kwa kitendo hicho hawakusita kuifungia zahanati
hiyo, pamoja na Zahanati zingine za mji wa Hoima zilizokuwa
zinaendeshwa chini ya viwango vinavyokubalika.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni