Naibu rais wa Kenya Bw. William Ruto
amemtaka kiongozi wa chama cha CORD, Raila Odinga kuacha kuhusisha
jina lake na kashfa za rushwa, na kumuonya kuwa yupo tayari kuanzisha
vita ya kisiasa na yeye.
Bw. Ruto amemtuhumu Odinga pamoja na
aliyekuwa msaidizi wake, Bw. Herbet Ojwang kwa kumuhisisha na rushwa
ya mradi wa shilingi bilioni 17 za Kenya, wa kuikarabati Hospitali ya
Rufaa ya Chuo cha Mafunzo Moi iliyopo Eldoret.
Mradi huo unachunguzwa na Kamati
Uwekezaji ya Umma (PIC) kutokana na tuhuma kuwa gharama ziliongezwa
na kwamba Ruto alitumia ushawishi wake kumtoa Bw. Ojwang katika mradi
huo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni