Idadi ya vifo vilivyotokana na moto
ulioteketeza kiwanda cha viatu nchini Philippine imefikia watu 72.
Polisi nchini humo wameahidi
kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na tukio hilo, huku
wafanyakazi wakidai uwepo wa mazingira duni ya afya pamoja na
kutofuatwa kwa viwango vya usalama.
Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi la
Philippine, Leonardo Espina amesema chanzo cha moto huo ni cheche ya
moto iliyoruka kutoka katika mashine ya kuchomelea na kutumbukia
kwenye kemikali zenye kulipuka karibu mlango wa kuingilia kiwandani.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni