Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa leo litafanya mkutano wa dharura wa majadiliano kuhusu
Burundi, baada ya jenerali mwandamizi kutangaza kuwa rais Pierre
Nkurunziza ameondolewa madarakani.
Ufaransa imeitisha mkutano huo ambao
utafanyika mara tu baada ya kikao cha mazungumzi yanayohusu Irak,
rais wa baraza hilo wa kutokea Lithuania ameeleza.
Taifa la Burundi limetumbukia zaidi
katika taharuki baada ya Jenerali Godefroid Niyombare, ambaye aliwahi
kuwa mkuu wa usalama wa taifa hilo mwenye nguvu kutangaza kung'olewa
rais Nkuruzinza, wakati rais akiwa nchini Tanzania.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni