.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 3 Mei 2015

PAMOJA NA KUPATA UPINZANI MKALI TOKA KWA MFILIPINO MANNY PACQUIAO, MAYWEATHER ATANGAZWA MSHINDI

Bondia Floyd Mayweather akimpelekea konde zito la mkono wa kushoto mpinzani wake Manny Pacquiao katika pambano lao la raundi 12 lililofanyika leo. 

Bondia Mmarekani Floyd Mayweather ameibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake Manny Pacquiao kwa pointi, katika pambano lao la raundi 12 lililofanyika alfajiri ya leo katika ukumbi wa MGM Grande Arena jijini Las Vegas nchini Marekani. 

Ushindi wa Mayweather ulifuatia majaji wote watatu kumpa ushindi, pamoja na pambano hilo kuonekana kuwa gumu kwani Manny Pacquiao alionekana wazi toka raundi ya kwanza akimtupia ngumi nzito mpinzani wake. 

Sasa Mayweather ameongeza taji lingine la WBO la uzito wa welterweight. Tayari Mmarekani huyo alikuwa na mataji ya ubingwa wa WBC na WBA. 

Mastaa kibao walifika ukumbiki kulishuhudia pambano hilo akiwemo Jay Z na mkewe Beyonce, 50 Cent, Justin Bieber, Mark Whalberg, Bradley Cooper na Donald Trump.
Bondia Floyd Mayweather akiwa amebanwa kwenye kona na mpinzani wake Manny Pacquiao katika raundi ya nne ya pambano hilo lililokuwa la raundi 12.
Kamata hiyo!! Pacman akimchapa konde la tumbo mpinzani wake Floyd Mayweather walipopambana katika ukumbi wa MGM Grande Arena, Las Vegas, Nevada nchini Marekani leo alfajiri.
Jamie Foxx akiimba wito wa taifa kabla ya pambano la Floyd Mayweather na Manny Pacquiao.
Mamia ya mashabiki wa mchezo wa ngumi waliokuwa wamefurika katika ukumbi wa MGM Grande Garden Arena wakichukua picha kupitia simu zao za mikononi wakati wa pamabano la Floyd Mayweather na Manny Pacquiao.
Mwanamitindo Cassie Ventura akiwa ameongozana na mwanamuziki P Diddy wakiingia katika ukumbi wa MGM Grande Arena kufuatilia pambano la Mayweather na Pacman. P Diddy ni rafiki wa karibu wa bondia Floyd Mayweather.
Mwanamuziki Beyonce Knowles akiwa na mumewe Jay Z wakifuatilia mpambano huo uliomalizika kwa Mmarekani Floyd Mayweather kutangazwa mshindi dhidi ya Pacman.
Bondia Floyd Mayweather akiwa na mikanda yake baada ya pambano lake na Pacman.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni