Maafisa wa polisi Jijini Washington
DC wanafanyiwa mafunzo ya namna ya kutumia vyoo vya umma bila ya
kusahau silaha zao vyooni.
Askari polisi katika Jiji hilo kuu
la Marekani, wameacha kwa bahati mbaya bastola zao katika majengo ya
vyoo vya umma mara tatu katika mwaka huu.
Moja ya bastola ya polisi iliyoachwa
chooni ilikutwa na mtoto na tayari mamlaka za jeshi hilo
zimewachukulia hatua maafisa hao kwa uzembe.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni