.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 22 Mei 2015

TAARIFA KUTOKA STAND UNITED FC

Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wakazi wa mkoa wa shinyanga,mikoa yote kanda ya ziwa na mashabiki wetu wote walioko nchi nzima na sehemu mbalimbali duniani kwa kutoa ushirikiano wao wa dhati kwetu katika michezo yetu ya ligi kuu tanzania bara msimu wa mwaka 2014-2015 iliomalizika tarehe 9/05/2015.

Tunasema asanteni sana kwa michango yenu ya hali namali,kifedha,kimawazo na ushauri pia,na hasa katika kipindi kigumu ambacho tumepitia.

Ulikuwa ni msimu wetu wa kwanza kushiriki katika ligi mengi tumejifunza na kuona mazuri na magumu katika ligi hii na soka la tanzania kwa ujumla,

tunaahidi kuiandaa timu kwa wakati muafaka na kwa weledi mkubwa lengo likiwa ni kufanya vizuri zaidi katika msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara.

Tunasisitiza kuwa bado hatujaanza kushughurika na swala la usajili wa mchezaji kwasasa na wala hatujafanya mazungumza na mchezaji yoyotekuhusu kumsajili, tunasubiri ripoti ya mwalimu wetu Mathias Rule kujua anapendekeza tufanye nini katika kuboresha timu yetu.

Tunakanusha vikali Taarifa ambazo zinasambaa hivi sasa kuwa tunafanya au tumefanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji ili kuwasajili akiwemo Juma Kaseja na Beki wa mtibwa sugar Salim Mbonde hatuna mazungumzo na wachezaji hao na hatutafanya usajili wowote bila kupata ripoti ya mwalimu.


Kama ripoti ya mwalimu itaelekeza tufanye usajili tutafanya hivyo na uongozi umejipanga kufanya usajili wenye tija na umakini wa kutosha kwa manufaa ya timu yetu ya Stand United fc.
 

Imetolewa na Idara ya Habari Stand United Fc.
Isaac Edward
Afisa habari.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni