Nchi ya Myanmar imefanikiwa kuwaokoa
wahamiaji zaidi ya 200 kwenye boti mbili katika ukanda wake wa
baharini unaopakana na Bangladesh.
Huu ni uokozi wa kwanza kufanywa na
Myanmar ambayo imekabiliwa na shutuma kwa kutofanya jitihada za
kutosha kusaidia wahamiaji waliokwama baharini.
Wengi wahamiaji ni kundi la waislam
wa jamii ya Rohingya wanaokimbia kuuwawa Myanmar, huku wengine
wahamiaji wanaoikimbia hali mbaya ya uchumi nchini Bangladesh.
Zaidi ya wahamiaji 3,000 wameingia
nchi za jirani za Malaysia, Thailand pamoja na Indonesia, ambazo
zimekubali kutoa msaada.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni