.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 22 Mei 2015

KUNDI LA DOLA YA KIISLAM (IS) LIMEUTWAA MPAKA WA AL-TANF BAINA YA SYRIA NA IRAK

Kundi la Dola ya Kiislam (IS) limeutwaa mpaka wa Syria na Irak uliokuwa chini ya serikali ya Syria, taarifa iliyotolewa na kundi linalofuatilia mgogoro wa nchi hiyo imesema.

Kundi hilo la Uangalizi wa Haki za Binadamu Syria limesema vikosi vya serikali vimejitoa kutoka katika mpaka wa al-Tanf uliopo Homs, wakati wapiganaji wa IS wakisonga mbele.

Kutwaliwa kwa mpaka wa al-Tanf inafuatia kundi la IS kuutwa mji wa kale wa Palmyra siku ya jana. Marekani imesema kupigana wapiganaji wa IS ni changamoto ngumu.

Kundi la Dola ya Kislam sasa linashikilia eneo la kilomita mraba 95 la Syri ambalo ni sawa na asilimia 50 ya eneo lote la taifa hilo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni