Wapigakura katika Jamhuri ya Ireland
leo watashiriki kupiga kura ya maoni juu ya kuhalalishwa ndoa za
jinsia moja.
Zaidi ya watu milioni 3.2 wataulizwa
iwapo wanataka kufanya mabadiliko katika Katiba ya nchi hiyo ili
kuruhusu ufungwaji wa ndoa za jinsia moja.
Kwa sasa duniani ni mataifa 19 tu
ambayo yamesharuhusu suala la kufungwa kwa ndoa za jinsia moja jambo
ambalo katika nchi nyingi za Afrika linachukuliwa kama ni kinyume na
mila na desturi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni