Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
amesema nchi yake inakabiliwa na tishio la shambulio la kigaidi
kutoka kundi la al-Shabaab la nchini Somalia.
Rais Nkurunziza ametoa kauli hiyo
wakati akiongea hadharani kwa mara ya kwanza mbele ya umma tangu
kushindwa kwa jaribio la kumpindua jumatano ya wiki iliyopita.
Katika hotuba hiyo Nkurunziza
hakuzungumzia lolote kuhusu jaribio hilo la mapinduzi, ambalo
limetokea baada ya wiki kadhaa za machafuko ya kumpinga asiwanie tena
urais.
Siku ya jumamosi watu 18,
walifikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya kusaidia
mapinduzi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni