Rais Uhuru Kenyatta, amelazimika
kuhairisha safari yake nchini Nigeria baada ya kuibuka hoja juu ya
idadi kubwa ya maafisa ambao walikokuwapo kwenye msafara wake.
Badala yake Naibu Rais wake William
Ruto amesafiri kumuwakilisha rais Uhuru katika sherehe za kuapishwa
kwa rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari hii leo.
Safari ya rais ilihairishwa baada ya
orodha ya maafisa 84 wa serikali watakaosafiri naye kuvuja katika
vyombo vya habari, na kuibua mjadala mkubwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni