Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika
Kusini amesema rais Jacob Zuma hatolazimika kurejesha fedha
zilizotumika kukarabati nyumba yake binafsi iliyopo nyumbani kwao
Nkandla.
Waziri Nathi Nhleko amesema
ukarabati huo, uliohusisha bwawa la kuogelea uligharimu randi milioni
4 sawa na dola 328,000, ulikuwa pia unahusisha msuala ya kuboresha
vifaa vya usalama.
Mwaka jana tume maalum ilibaini kuwa
rais Zuma, alijinufaisha kimamakosa katika kukarabati nyumba yake
hiyo kwa kutumia fedha za umma. Rais Zuma amekosolewa mno kwa hilo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni