Mahakama ya Juu Nchini China imesema
imetekeleza adhabu ya kuuwawa kwa mwalimu wa shule ya msingi
aliyetiwa hatiani kwa kubaka na kuwadhalilisha kingono watoto wakike
26.
Mwalimu Li Jishun alitenda makosa
hayo kati ya mwaka 2011 hadi 2012 wakati alipokuwa akifundisha kwenye
shule ya kijijini katika mkoa wa Gansu.
Matendo hayo ya kikatili aliwafanyia
watoto wa kike wenye umri wa kuanzia miaka 4 hadi 11 kwa mujibu wa
nakala ya mahakama ya juu ya China.
Kumekuwepo na matukio 7,000 ya
udhalilishaji kingono watoto nchini China katika miaka ya hivi
karibuni na matukio hayo yanazidi kuongezeka.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni