Mshindi wa uchaguzi mkuu wa mwezi
Machi nchini Nigeria Muhammadu Buhari ameapishwa kuwa kiongozi wa
taifa hilo maarufu la Afrika.
Rais Buhari anakuwa kiongozi wa
kwanza wa upinzani kushinda uchaguzi wa urais Nigeria tangu taifa
hilo lipate uhuru wake mwaka 1960.
Buhari ametwaa madaraka kutoka kwa
Goodluck Jonathan, ambaye amemtaka aiunganishe nchi hiyo dhidi ya
tishio la kundi la Boko Haram.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni