Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo inashuka dimbani kucheza mchezo
wake wa pili dhidi ya timu ya Taifa kutoka Madagascar, mchezo
utakaochezwa katika uwanja wa Royal Bafokeng majira ya saa 12 jioni kwa
saa za Afrika Mashariki.
Taifa
Stars inahitaji kupata ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Madagascar
ili kufufua matumaini ya kuweza kusonga mbele katika hatua inayofua ya
Robo Fainali.
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars akiongelea mchezo wa leo amesema, makosa
yaliyojitokeza katika mchezo dhidi ya Swaziland yamefanyiwa kazi na
anaamini vijana wake watafanya vizuri.
“Mchezo
wa Swaziland tulipata nafasi nzuri za kufunga, lakini washambuliaji
wangu hawakuwa makini kuzitumia nafasi hizo, tatizo la kupoteza nafasi
nyingi limefanyiwa kazi na nina amini leo vijana watafanya vizuri”
alisema Nooij.
Aidha
Nooij amesema anataarajia mchezo kuwa mgumu kutokana na Madagascar
kuhitaji ushindi wa pili mfululizo, baada ya kuifunga Lesotho katika
mchezo wa awali, Nooij ameahidi kufanya vizuri katika mchezo huo.
Mchezo huo utakuwa moja kwa moja (Live) katika kituo cha Superspot SS4, na SS9.
Naye
kiungo wa Taifa Stars, Said Juma Makapu anarejea nyumbani leo usiku kwa
usafiri wa Shirika la ndege la Fastjet kwa ajili ya kufanyia vipimo
zaidi na matibabu, anatarajiwa kuondoka uwanja wa O.R. Tambo saa 5 usiku
kufika uwanja wa JK Nyerer saa 8 usiku.
UCHAGUZI MKUU COASTAL UNION JULAI 5
Kamati
ya Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limetangaza
Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga utafanyika
tarehe 05, Julai 2015.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Melchesedek Lutema ametoa ratiba
ya mchakato mzima wa uchaguzi huo, ambapo tarehe 21-22 Mei mwaka huu
zitatangazwa nafasi zote zinazogombewa.
Kwa
mujibu wa kalenda hiyo ya Uchaguzi, tarehe 23-30, Mei 2015 itakua ni
kipindi cha uchukuaji fomu kwa wagombea wote na kuzirudisha, wakati Juni
Mosi mpaka Juni 04, 2015 ni kipindi cha mchujo wa awali kwa wagombea.
Juni
05, 2015 Kamati ya Uchaguzi itatoa orodha ya awali ya wagombea, Juni
7-9, 2015 itakua ni kipindi cha kupokea na kuweka pingamizi kwa
wagombea, na Juni 10-11 ni kupitia mapingamizi yote.
Julai 02 -04, 2015 ni muda wa kampeni kwa wagombea wote na uchaguzi mkuu utafanyika tarehe 05, Julai 2015.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni