Vyama vingi vya soka vya mataifa ya
Ulaya vimeonyesha kukerwa na kuchaguliwa tena rais wa Shirikisho la
Soka la Duniani (Fifa) Sepp Blatter.
Mkuu wa Chama cha Soka cha Denmark,
amesema ushindi huo ni kushindwa kwa uwazi, wakati Mwenyekiti wa
Chama cha Soka Uingereza (FA) amesema anaweza kuunga mkono kususia
kombe la dunia.
Hata hivyo waandaaji wa michuano ya
kombe la dunia lijalo nchi ya Urussi, imesema imefurahishwa na
kuchaguliwa tena na Blatter.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni