Vikosi vya ulinzi Kenya jana jioni
vimetibua jaribio la shambulio la kigaidi lililopangwa na wapiganaji
wa kundi la Al-Shabaab kwenye kijiji cha Yumbis katika kaunti ya
Garissa.
Waziri wa Mambo ya Ndani imesema
wanakijiji walitoataarifa kwa vikosi vya usalama, kuwa wameona
wapiganaji wenye siala majira ya saa 12 jioni.
Msemaji wa Wizara hiyo Mwenda Njoka
ameleza kuwa vikosi vya usalama viliwavamia wapiganaji hao na
kupambana nao, hata hivyo hakukuwa na taarifa za kuwepo mtu
aliyejeruhiwa.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Kenya Joseph
Boinnet, amesema wapiganaji wa Al-Shabaab, wanawaghasi wananchi,
lakini vikosi vya usalama vimewatimua.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni