Shirikisho la Kimataifa la Haki za
Binadamu limesema vikosi vya ulinzi vya Misri vinatumia shambulio la
ngono dhidi ya kundi la watu wengi wanaoshikiliwa.
Ripoti ya shirikisho hilo imeeleza
wanaume, wanawake na watoto wamekuwa wakidhalilishwa ili kudhibiti
maandamano ya umma.
Wengi wa wanaoshikiliwa hufanyiwa
vipimo vya ubikira, kubakwa pamoja na kubakwa genge la la watu baada
ya kukamatwa. Wizara ya Mambo ya Ndani Misri imesema itatoa taarifa
yake baada ya kuiona ripoti hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni