Umoja wa Mataifa, umesema watoto
Sudan Kusini ambao ni wadogo hadi kufikia umri wa miaka saba
wameuwawa, kutekwa na kubakwa katika machafuko ya hivi karibuni.
Manusura wa shambulio hilo
lililotokea katika jimbo al Unity wanaamini limetekelezwa kundi la
wapiganaji wa Sudani Kusini.
Mapigano baina ya serikali na waasi
yamesambaa katika wiki za hivi karibuni, na kuwafanya watu 100,000
kukosa makazi.
Shirika la Msalaba Mwekundu limeonya
uwezekano wa kuwepo kwa mgogoro wa chakula wakati huu maelfu
wakikimbia kambi kuu ya waasi ya Leer.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni