Maafisa polisi sita nchini
Afghanistan wamehukumiwa kifungo cha jela mwaka mmoja kwa kushindwa
kumlinda mwanamke aliyeuwawa mwezi Machi Jijini Kabul mwezi Machi.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka
28, aitwae Farkhunda alipigwa hadi kufa kutokana na kutuhumiwa
kuunguza nakala ya Kuraan, ingawa mashahidi wamesema hakufanya hivyo.
Mapema mwezi huu wanaume wanne
walihukumiwa adhabu ya kifo kwa kumuua mwanamke huyo na wengine nane
wamehukumiwa vifungo vya jela.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni