Zaidi ya watu 50, wamekufa katika
maporomoko ya ardhi katika mkoa wa Antioquia kaskazini magharibi mwa
Colombia.
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos
amesema mamlaka zake bado hazina taarifa sahihi za watu ambao hadi
sasa hawajulikni walipo.
Mvua kubwa zinazonyesha
zimesababisha mto Liboriana katika mji wa Slagar kupasuka kingo zake
na kusababisha maporomoko ya ardhi.
Vijiji vingi vya Santa Margarita,
vilivyopo kusini magharibi mwa mji mkuu Medellin vimesombwa maji
baada ya mto huo Liboriana kupasuka kingo zake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni