Watu 2,000 wamekimbilia mahali
salama kufuatia maporomoko ya ardhi, magharibi mwa Nepal, ambako
kunakingo za kuzuia maji.
Mto Kali Gandaki katika wilaya ya
Myagdi karibu kilomita 140 kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa
Kathmandu, umetengeneza kina kirefu na kukua ziwa jipya.
Idadi kadhaa za maporomoko ya ardhi
yameikumba Nepal tangu tetemeko la ukubwa wa alama 7.8 Aprili 25
ambalo liliuwa watu zaidi ya 8,000 na kujeruhi wengi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni