Watu wenye silaha nchini Pakistan
katika mkoa wa Balochistan wameshambulia mabasi mawili na kuua abiria
wapatao 19.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Mkoa huo
Sarfraz Bugti, wapiganaji hao ambao hawakutambulika walipanda mabasi
hayo yaliyokuwa yakisafiri kuelekea Karachi jana usiku.
Wapiganaji hao baadae waliwamuru
abiria kushuka chini na kuwapiga risasi. Mkoa wa Balochistan umekuwa
na mapigano baina ya kundi linalotaka kujitenga na vikosi vya
serikali.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni