Nchi ya Italia imeokoa zaidi ya wahamiaji 3,300 waliokuwa wakijaribu kukatiza bahari ya Mediterranean siku ya jana, kikosi cha ulinzi cha pwani kimesema.
Katika moja ya operesheni hiyo miili
ya watu 17 imepatikana kwenye boti tatu, na watu 217 waliokuwa kwenye
boti hizo wameokolewa.
Walinzi wa pwani wamesema walipata
simu za kuomba msaada kutoka kwenye boti 17 tofauti hapo jana.
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji
(IOM) limesema watu 1,826 wamekufa wakijaribu kukatiza bahari ya
Mediterranean kutafuta maisha tangu mwaka 2015.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni