Waziri Mkuu wa Malaysia Najib Razak amesema nchi yake itafanya zoezi la kuwaokoa wahamiaji wa Rohingya waliopo katika maboti kwenye ziwa la Andaman.
Amesema pia misaada ya kibinadamu pia itatolewa kwa wahamiaji waliofika nchi kavu na waliobakia baharini. Zaidi ya wahamiaji 7,000 inaaminika bado wapo baharini.
Kauli hiyo ya Waziri Razak imekuja wiki kadhaa baada ya mamlaka za nchi kukataa boti hizo kuingia nchini na kuzifukuza katika mipaka ya majini ya Malaysia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni