KUELEKEA Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Coastal Union tayari maandalizi
yameanza kukamilika kwa asilimia kubwa ambapo jumla ya wagombea kumi na tano wamejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi mbalimbali zauongozi.
Akizungumza leo ,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema katika uchaguzi mkuu nafasi ambazo wagombea wamejitokeza ni Mwenyekiti
ambapo nafasi hiyo amejitokeza Dokta Ahmed Twaha akiwa hapa mpinzani.
Nafasi ya makamu Mwenyekiti wamejitokeza wagombea wawili ambao ni
Salim Amiri na Hussein Abdull Ally ambao watachuana ili kuweza kupatikana mshindi ambayo atachukua nafasi hiyo.
Aidha amesema kuwa katika nafasi ya Kamati ya utendaji wamejitokeza wagombea kumi na mbili ambao watachuana na kubaki wajumbe watano watakaounda kamati ya utendaji.
Amewataja waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni Albert Clement Peter,Omari Mwambasha,Waziri Mohamed,Mohamed Ally “Dondo”,Mohamed Maulid Rajabu,Abubakari Ahmed Machai,Aggrey Ally Mbapu,Hassani Omari
Bwana.
Wengine ambao wamejitokeza kuwania nafasi hiyo kuwa ni Abdallah Zuberi
Ally “Unenge”,Hassani Ramadhani Muhsin,Albert Clement Peter,Hussein
Ally Mwinyi Hamis na Salim Abasi Perembo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni