Mkuu wa maabara chakula TBS Stella E. Mrosso aliye Mwakilisha Mgeni rasmi katika hafla hiyo akimkabidhi rasmi fomu za shindano la mama shujaa wa chakula Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster kwa ajili ya kuanza kufanya maamuzi.
Shindano la mama shujaa wa chakula limeingia katika hatua mpya baada ya zoezi la kukusanya fomu za washiriki kutoka mikoa mbalimbali nchini kupitiwa na majaji kwa ajili ya mchujo ambapo washiriki 18 watapatikana kisha baadaye 15 bora ambao wataingia kijijini kwa ajili ya mchakato wa kugombea nafasi ya mama shujaa wa chakula mwaka 2015.
Zoezi la kusahihishwa fomu limezinduliwa mapema leo hii na mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TBS, Joseph Masikitiko ambaye ni Mkuu wa Maabara na Chakula TBS, Bi. Stella Mrosso akiwa sambamba na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania, Jenny Foster na majaji watakaopitia zoezi zima la mchujo wa fomu hizo.
Akizungumza na wageni waandishi wa habari katika uzinduzi huo Mkuu wa Maabara na Chakula, Bi. Stella Mrosso alilisifu shirika la Oxfam kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za wanawake, umiliki wa ardhi na kuhamasisha uzalishaji wa chakula kwa wazalishaji wadogo wadogo.
Bi. Stella alisisitiza kuwa kila mzalishaji anapaswa kuzalisha bidhaa bora ili kushindana na soko la ndani na la nje huku akifafanua kuwa kwa kupitia SIDO, TFDA na Wizara ya Afya, wazalishaji wadogowadogo watakuwa na uwezo wa kupata kibali kutoka TBS bure na kuongeza kuwa wakina mama nchini watumie shindano la mama shujaa wa Chakula kama chachu ya kujitokeza kwa wingi katika mashindano yanayofuata huku wengine wakijifunza uzalishaji bora kupitia mashindano hayo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni