.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 9 Juni 2015

DK. MWELE MALECELA ACHUKUWA FOMU LEO ZA KUWANIA URAIS KWA TIKETI YA CCM

Mkurugenzi wa taasisi ya Taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu Dkt. Mwelechele Ntuli Malecela amechukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye nafasi ya urais.

Dkt. Malecela ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani John Malecela amekuwa mwanamke wa pili kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia CCM baada ya Balozi Amina Salum Ally kuchukua fomu wiki iliyopita.

Dkt Malecela amesema kuwa kama atapewa ridhaa ya kuwania nafasi ya urais kupitia CCM atawawezesha wanawake nchini kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za maamuzi kwani awamu hii ya nne imewapa upendeleo wa kutosha.

Amesema kwa sasa hawezi kuahidi kuwa atawafanyia nini Watanzania hadi pale atakapopewa ridhaa na chama chake ambapo atatekeleza vipaumbele vilivyoko katika ilani ya chama chake, hata hivyo amesema atahakikisha kuwa huduma za afya, elimu ya ufundi, uchumi na kuudumisha muungano ambayo ni tunu ya Taifa vinatekeleza kwa uhakika.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni