Bi Moza Moh'd Khamis anapenda tena kutoa shukurani za dhati
kwa wale wote waliochangia kwa hali na mali kwa mtoto wake Moh'd Said
Moh'd, kwenda kufanyiwa matibabu ya
upandikizaji wa figo, nchini India.
Mapema asubuhi ya leo Bi Moza aliongea na blog ya
swahilivilla ili kutoa taarifa kwa kukamilika safari yake ya kwenda nchini
India pamoja na kutaka tumuombe Dua za kumtakia kila la kheri katika safari hiyo.
Moh'd Said Moh'd ameondoka leo Jumanne Juni 9, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam kuelekea Nchini India kwaajili ya matibabu yake.
Napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Tanzania Bloggers
Network (DMV) na waTanzania wote waishio Nchini Marekani, kumtakia kila la
kheri Ndugu yetu Moh'd Said Moh'd katika
matibabu yake huko Nchini India.
M/Mungu amjaalie wepesi katika safari yake na ampe afuweni
na mafanikio katika mipangilio yote matibabu yake. Ameen.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni