Idara ya sheria ya Afrika Kusini
inajiandaa kwa ajili ya malumbano ya kisheria katika Mahakama Kuu ya
Pretoria, huku kukiwepo kwa taarifa kuwa rais Omar al-Bashir wa Sudan
ameondoka Afrika Kusini jana usiku.
Licha ya taarifa za kuondoka
kutothibitishwa, suala la kuondoka Afrika Kusini litakuwa ni kinyume
na amri ya Mahakma Kuu ya Pretoria ambayo jana mchana iliishinikiza
mamlaka ya Afrika Kusini kutomruhusu rais al-Bashir kutoondoka
nchini.
Msemaji wa Idara ya sheria Wakili
Mthunzi Mhaga, amesema hakuna uthibitisho kuwa rais Al-Bashir
ameondoka nchini humo.
Wakati al-Bashir akiendelea
kuhudhuria vikao cha Umoja wa Mataifa kwa uhuru si mbali sana kutoka
Mahakama Kuu ya Pretoria, vyombo vya haki za binadamu vimekuwa
vikipambana kuhakikisha anakamatwa.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni