Wakati wa Rais wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni ( FIFA ) Sepp Blatter akitangaza kusudio lake la kujiuzulu kufuatia kashfa ya ufisadi inayomkabili, maafisa wa FBI wametangaza kumchunguza rais huyo.
Blatter aliyeshinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho hilo uliofanyika hivi karibuni mjini Zurich, Switzerland ameshuhudia shutuma mbalimbali toka kwa wadau wa soka hasa barani Ulaya kufuatia kashfa ya rushwa inayoliandama shirikisho hilo.
Tayari maafisa saba ( 7 ) wa Fifa wamekatwa na sasa wanachunguzwa na FBI kwa kashfa ya rushwa.
Blatter mwenye umri wa miaka 79 ameitisha kikao cha dharura mjini Zurich yalipo makao makuu ya Fifa, na kusema uchaguzi mwingine uhenda ukafanyika mwezi Disemba mwaka huu au Machi mwakani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni