Tamasha la Nyota wa Pop Jennifer
Lopez nchini Morocco, limepelekea kutolewa wito wa kutaka waziri wa
mawasiliano wa nchi hiyo ajiuzulu.
Mjumbe mashuhuri wa Chama Tawala cha
Haki na Maendeleo, amesema shoo ya mwanamuziki huyo katika tamasha la
Mawazine Jijini Rabat, ilivunja maadili ya umma.
Waziri wa Mawasiliano Mustapha
Khalfi, alikosolewa kwa kuruhusu tamasha hilo kurushwa kwenye kituo
cha televesheni cha umma. Hata hivyo amegoma kujiuzulu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni