Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitembelea shamba la mkulima bora wa migomba, Eurius Kishinju katika Kata ya Mabira, wilayani Kyerwa, mkoani Kagera.
Kinana ambaye ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye wanaanza rasmi ziara mkoani Kagera, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kishinju ambaye ana shamba la migomba heka 3 mchanganyiko na kahawa, kwa mwezi huuza mikungu 43 kwa mwezi ambapo kila mkungu huuza kwa sh. 10,000, hivyo kujipatia kitita cha sh. 430,000, pia huvuna magunia 25 ya kahawa, ambapo sehemu ya mapoato hayo amejengea nyumba ya kisasa na kusomesha watoto wake wawili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
Komredi Kinana akikagua shmba bora la migomba na kahawa katika Kata ya Mabira, linalomilikiwa na mkulima Kishinju.
Komredi Kinana akikagua shmba bora la migomba na kahawa katika Kata ya Mabira, linalomilikiwa na mkulima Kishinju.
Katibuwa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kikukuru, Katika Kata ya Mabira, wilayani Kyerwa. Mabira Kikukuru
Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mabira, wilayani Kyerwa, mkoani Kagera.
Wananchi wakimsalimia Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana alipokwenda kukagua Zahanati yaKijiji cha Kigorogoro wilayani Kyerwa, Kagera.
Wananchi wakiwa na furaha wakati wa kumlaki Komredi Kinana katika Kijiji cha Kigorogoro, wilayani Kyerwa
Komredi Kinana akihutubia alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Soko la Kimataifa la Murongom wilayani Kyerwa, ambao hivi sasa umesimama.Soko hilo lipo mpakani mwa Tanzania na Uganda.
Wananchi bwa Kata ya Kaisho, Kijiji cha Kibingo wakishangilia walipokuwa wakimlaki Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana ambaye alifanya ziara katika eneo hilo kuzindua mradi wa maji na kuhutubuia wananchi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, ,AKIWA AMESIMAMA KWENYE GARI AKIANGALIA MWENENDO WA MKUTANO WA HADHARA KATIKA KIJIJI CHA KIBINGO, WILAYANI KYERWA.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni