Serikali ya Tunisia imelikamata
kundi la watu kuhusiana na mauaji ya watu 38, wengi wao wakiwa ni
watalii katika fukwe ya Sousse siku ya Ijumaa.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tunisia,
Mohamed Gharsalli amesema kuwa kikosi cha askari
1, 000 sasa kitawekwa kulinda fukwe
za nchi hiyo.
Mawaziri watatu wa Ulaya wameweka
mashada ya maua katika eneo lililotokea la mashambulio hayo katika
kuonyesha mshikamano dhidi ya vitendo vya kigaidi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni