Watu wapatao nane wamejeruhiwa,
wawili miongoni mwao wakijeruhiwa vibaya baada ya mwanaume mmoja
kujichoma moto ndani ya treni ya mwendo kasi ya Shinkansen nchini
Japan.
Msemaje wa Shirika la Reli la Japan
amesema abiria huyo alijimwagia mafuta mwilini mwake na kisha
kujichoma moto akiwa ndani ya treni hiyo.
Treni hiyo ilikuwa ikitokea Tokyo
kwenda Osaka wakati tukio hilo la mtu kujichoma moto lilipotokea
karibu na mji wa Odawara.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni