Mwanamuziki Lionel Richie amevutia
umati mkubwa wa watu katika tamasha la mwaka huu la Glastonbury,
ambapo karibu watu 100,000 inasemekana wamemuangalia mwanamuziki huyo
nguli duniani.
Jukwaa la Pyramid lililotumika
kufanyika tamasha hilo lilivutia umati watu waliokuja kumuona Lionel
Richie akitumbuiza vibao vyake vikali kama vile Dancing on the
Ceiling, Hello pamoja na Say You Say Me.
Tamasha hilo la muziki lilifungwa na
wakongwe wa muziki wa rock The Who ambao waliimba vibao vyao vikali
katika jukwaa la Pyramid ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya mwisho ya
kimuziki duniani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni