Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, amesema sanaa ya muziki ina nafasi kubwa ya kuendeleza amani na maelewano duniani.
Amesema kupitia sanaa hiyo wanamusiki kutoka pembe tofauti za dunia wamekuwa wakikutana kubadilishana uzoefu na kusoma tamadunia za kila upande, jambo ambalo husaidia pia kuzitangaza nchi na tamaduni zao katika ramani ya dunia.
Dkt. Shein ameeleza hayo huko chuo cha musiki Forodhani, katika hotuba yake iliyosomwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa siku nne wa muziki kwa nchi za jahazi.
Amesema Zanzibar ikiwa nchi yenye historia ya muziki hasa wa Taarab, imekuwa ikijifunza kutoka kwa wanamuziki wa nchi nyingi duniani zikiwemo India, Misri na nchi za Afrika kama vile Nigeria, Congo na Comoro, jambo ambalo limeifanya Zanzibar kuwa na uhusiano wa karibu wa kiutamaduni na nchi hizo.
Amefahamisha kuwa Zanzibar inakusudia kuibua na kuendeleza vipaji vya wanamuziki wachanga, na kwamba mkutano huo utatoa fursa kwa wanamuziki wa Zanzibar kujifunza mbinu mbali mbali za muziki zitakazosaidia kukuza vipaji vyao.
Naye Mkurugenzi wa Chuo cha Muziki Zanzibar bibi Fatma Kilua, amesema kufanyika kwa mkutano huo hapa Zanzibar ni fursa pekee kwa wanamuziki wa Zanzibar kujifunza na kuitangaza katika fani hiyo.
Kwa upande wake muandaaji wa mkutano huo Profesa Raymond Vogals amesema, sanaa ya muziki imekuwa ikipata maendeleo makubwa duniani, na tayari wanamuziki kadhaa wameshahitimu shahada ya uzamivu (PHD) katika fani hiyo wakiwemo pia kutoka bara la Afrika.Hassan Hamad (OMKR)
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni