Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla akihutubia wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya.
Mbunge wa Mvomero Mh Amos Makalla amekabidhi pikipiki tano kwa kata mpya
tano za Chama cha mapinduzi ili kuwasaidia watendaji na viongozi wa
Chama kufanya kazi za Chama kwa wepesi na ufanisi.
Akimkambidhi pikipiki hizo, Mbunge wa Mvomero alimueleza mwenyekiti wa
wilaya ya Mvomero ndugu Abdalah Mtiga, kuwa msaada huo ni muendelezo wa
kukisaidia Chama wilaya ya Mvomero kwani awali alisaidia pikipiki 23, na
hizo 5 inafanya jumla ya pikipiki alizosaidia Chama ni 28 zenye thamani
ya sh 56,000,000.
Akipokea msaada huo, mwenyekiti wa wilaya ndugu Abdalah Mtiga alimshukuru
sana mbunge huyo kwa Moyo wake wa kukipenda Chama, kwani ni wabunge
wachache sana wenye Moyo kama wa mbunge Amos Makalla.
Aliwataka
watendaji kutunza pikipiki hizo na zitumike kwa shughuli za chama na si
vinginevyo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni