Mafuriko makubwa yamelikumba Jiji
Kuu la Tbilisi nchini Georgia na kuuwa watu wanane, ambapo maafisa wa
nchi hiyo wamewaonya wananchi kutotoka nje ili kuepuka kukutana na
wanyamapori waliotoroka kwenye eneo la kufugia wanyamapori.
Wanyama hao ambao hawajulikani
walipo ni duma, simba, dubu pamoja na mbweha, ambapo pia inasadikiwa
kwamba muangalizi wa wanyama hao amekufa.
Kiboko mmmoja amefanikiwa
kudhibitiwa katika eneo kuu la mapumziko la Jiji Tbilisi na kupigwa
na bunduki yenye sindano ya usiongizi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni