.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 14 Juni 2015

WATU 57 WAKAMATWA MOROCCO KWA KUVUJISHA MAJIBU YA MITIHANI

Makumi ya watu wamekamatwa nchini Morocco kwa kutenda kosa la kuuza majibu ya mtihani wa taifa wa kidato cha sita katika hali ambayo pia imepelekea majibu ya mitihani miwili kuwekwa kwenye ukurasa wa Facebook.

Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa amesema watu 57 wamekamatwa katika miji 15 wakiuza majibu ya mtihani ambapo kwa baadhi ya mitihani majibu yalikuwa yakitumwa kwa wanafunzi kwa kutumia ujumbe mfupi wa maandishi.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kwamba watu waliokamatwa wanatuhumiwa kutoa majibu yaliyoandikwa tayari kwa wanafunzi na kujipatia fedha.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni