.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 14 Juni 2015

BONDIA MMAREKANI DEONTAY WILDER AMETETEA TAJI LAKE LA UZITO WA JUU DUNIANI LA WBC

Bondia Mmarekani Deontay Wilder ametetea taji lake la uzito wa juu duniani la WBC baada ya kufanikiwa kumtwanga kwa knockout bondia Eric Molina katika raundi ya tisa.

Bondi huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye alimpiga Bermane Stiverne mwezi Januari na kuwa Mmarekani wa kwanza kutwaa taji la uzito huo tangu mwaka 2007, hajapigwa katika mapambano 34 aliyocheza.

Molina, mwenye umri wa miaka 33, ambaye amepoteza michezo yake miwili kati ya 25, aliangushwa chini katika raundi ya nne, na mara mbili tena katika raundi ya tano, ambapo alisalimu amri katika raundi ya tisa ndipo na kushindwa kuendelea na pambano.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni