Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wazee na Viongozi wa Muyuni “A
“ na Muyuni “ B “ kabla ya kuzungumza nao kujadili tatizo la
migogoro ya Ardhi.
Baadhi ya Viongozi wa Shehia za
Muyuni “A “ na Muyuni “ B “ wakimsikiliza Balozi Seif hayupo
pichani wakati wa kujadili changamoto zinazowakabili za migogo ya
Ardhi { Hifadhi ya Misitu } ndani ya Shehia hizo wa kwanza kutoka
kushoto ni Afisa Tawala wa Wilaya ya Kusini Bi Kibibi Mwinyi Hassan.
Balozi Seif akizungumza na Wazee na
Viongozi wa Muyuni “A “ na Muyuni “ B “ baada ya kupokea
changamoto zinazowakabili za migogoro ya ardhi. Kulia ya Balozi Seif
ni Mkuu wa Mkopa wa Kusini Unguja Dr. Idriss Hijja na Kushoto yake
ni Mwenyekiti wa Kikao hicho Diwani Mstaafu wa Muyuni Bwana Abdulla
Hija Abdulla. Picha na – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
haipendelei kuona Wananchi katika baadhi ya shehia wanalumbana na
kufikia hatua ya kuhitilafiana katika mambo ambayo wakiamua kukaa
pamoja katika kuyajadili kwa njia ya vikao yanaweza kurekebishika
bila ya kutumika nguvu za Serikali Kuu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wazee na
Viongozi wa Shehia za Muyuni “A “ na Muyuni “B” katika kikao
cha kujadili matatizo yaliyojitokeza baina ya Wananchi dhidi ya
viongozi wao wa shehia hizo.
Balozi Seif Ali Iddi alisema tabia
ya baadhi ya wananchi hasa Vijana kutumia njia ya mkato katika
maamuzi yao ya kurejesha Kadi za uanachama ni udhaifu unaofa
kuepukwa kwa vile hauwezi ukatoa suluhu ya tatizo linalolalamikiwa na
Wananchi hao.
Alisema maisha ya amani na utulivu
ndio yanayotegemewa na Serikali Kuu kuendelea kushamiri ndani ya
Shehia hapa nchini ambazo zinawajibika kufanya kazi kwa umakini.
Balozi Seif alieleza kuwa Sheha wa
Shehia yoyote ile hapa Zanzibar ni mtumishi wa Serikali kwa mujibu wa
Katiba ya Zanzibar asiyepaswa kuhusika na vitendo vinavyoashiria
vurugu ndani ya eneo lake.
Mapema Diwani Mstaafu wa Wadi ya
Muyuni Bwana Abdulla Hijja Abdulla ambae ndie mwenyekiti wa Kikao
hicho alielezea matatizo mengi yanayowasumbuwa Wananchi hao wa Muyuni
“ A “ na Muyuni “ B “ hasa lile la hifadhi ya msitu ambalo
waliamuwa kuianzisha kwa hatma yao ya baadaye.
Bwana Abdulla alisema uchelewaji wa
kuchukuliwa hatua za kisheria katika ngazi za Shehia, Wilaya na Mkoa
dhidi ya watu waliomua kuvamia hifadhi hiyo ndilo tatizo kuu
lililoibua mtafaruk kati ya Wananchi hao wa Uongozi wa Shehia hizo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kusini Nd.
Khamis Jabir Makame alisema alilazimika kulitembelea eneo la Mgogoro
wa Ardhi katika eneo la Hifadhi ya Muyuni muda mfupi uliopita ili
kujionea hali halisi ya kile kinacholalamikiwa.
Nd. Jabir alikieleza kikao hicho
kwamba akiwa pamoja na Viongozi wenzake wa Wilaya alibaini kuwepo kwa
miti ya kudumu iliyooteshwa kwa muda mrefu katika eneo hilo pamoja na
Miti ya matunda ambayo tayari imeaanza kuzaa.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
19/6/2015.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni