.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 18 Juni 2015

MAREKANI KUTOA NOTI YA DOLA KUMI YENYE SURA YA MWANAMKE

Idara ya hazina ya Marekani, imesema noti ya dola 10 inayobuniwa kwa mara ya kwanza itakuwa na sura ya mwanamke, lakini haijaamuliwa mwanamke huyo atakuwa nani.

Noti hiyo mpya ya dola kumi itatolewa mwaka 2020 katika kuadhimisha miaka miaka 100 ya mabadiliko ya 19 ya Katiba, ambayo yalimpatia mwanamke haki ya kupiga kura.

Hazina ya Marekani itahitaji michango ya wananchi katika uchaguzi wa mwanamke huyo ambaye anamchango mkubwa katika demokrasia ya kuhusisha makundi yote.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni