Ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema
idadi ya watu wasiokuwa na makazi kutokana na vita, migogoro ama
mauaji ya visasi imefikia rekodi ya juu ya watu milioni 60 duniani
kote.
Taarifa ya Shirika la Umoja wa
Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi Duniani, UNHCR, imesema idadi ya
watu waliolazimishwa kukimbia nyumba zao imeongezeka kwa watu milioni
8.3 kutoka mwaka jana.
Machafuko ya nchini Syria inaonekana
kama chanzo kikuu cha ongezeko la idadi ya watu wasio na makazi
duniani. Mkuu wa shirika la UNHRC Antonio Guterres amesema dunia
imechafuko.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni