Pongezi hizo alizitoa jana mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya kata
ya Mhonda waliokuwa na kikao na mbunge wao.
Katika maelezo yake, mkuu wa chuo aliwakaribisha ukumbini hapo kwa kumpongeza mbunge kwa mchango
mkubwa ambapo alisema,
" viongozi wa kata jana mliniomba kukodi ukumbi
tukawaruhusu, ila kwakuwa mbunge yupo hapa naomba niseme na hata viongozi
wa wizara ya Elimu niliwaambia kuwa mdau mkubwa aliyechangia vifaa
ikiwemo nondo, saruji na mabati zaidi ya asilimia 70 ya ujenzi ni Mhe
Makalla, tunakushukuru na kama utakavyoona jina la ukumbi tumeandika hapa
inaitwa Makalla Hall, hakika tunakushukuru sana" alisema.
Akiwahutubia wajumbe wa halmashauri kuu ya kata ya Mhonda, Mh Makalla aliwaambia
kuwa anamshukuru mkuu wa chuo kwa pongezi, na wajumbe wameona kwa macho
ukumbi ulivyo mzuri na kwa kuboresha mazingira hayo sasa hata chuo
kimepata hadhi kutoka kutoa cheti sasa wameruhusiwa wameanza kupokea
wanafunzi wa diploma.
Amewaeleza amefanya mambo mengi ya maendeleo katika sekta ya Elimu
ikiwemo kuchangia ujenzi wa sekondari zote jimbo la Mvomero, amesaidia
vitabu vya sayansi katika sekondari zote wilaya ya Mvomero, amechangia sh
21,000,000 ujenzi wa Maabara kwa sekondari 21 kila sekondari shilingi
milioni moja, na pia amewasaidia kompyuta na printa Saccos ya walimu
wilaya ya Mvomero.
Katika tukio la aina yake, mbunge huyo alijumuika na wanachuo kupata chakula
cha pamoja kitendo kilichowafurahisha viongozi wa Chuo, Chama na
wanachuo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni